Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi amewataka wananchi wa wanaosafiri mara kwa mara kwa ajili ya
harakati zao za maisha kuchukua vyandarua na kuvitumia wanapokuwa safarini ili
kujikinga na maradhi ya Malaria.
Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya
Malaria Duniani katika viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar, Balozi Seif alisema
licha ya Zanzibar kuwa na kiwango cha chini ya asilimia moja cha Malaria,
utafiti unaonyesha watu wanaogunduliwa kuugua maradhi hayo hivi sasa ni wale
wenye utaratibu wa kusafiri nje ya Zanzibar.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imedhamiria kwa dhati kuimarisha afya za wananchi na itaendelea kuboresha
huduma za afya sehemu zote na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo.
Hata hivyo alisema wakati Zanzibar inajivunia
mafanikio katika vita dhidi ya Malaria bado maradhi ya Kipindupindu yanaendelea
kuwa tishio kwa wananchi na kuwataka kufuata maelekezo yanayotolewa na
wataalamu wa afya.
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Afya Juma Malik
Akili alisema katika kumaliza Malaria kuanzia tarehe 25 mwezi huu watatoa
vyandarua 760,000 vilivyotiwa dawa bure kwa wananchi katika Wilaya zote
za Zanzibar.
Amewashauri wananchi kuvitumia vyandarua hivyo
kikamilifu kwani inaonekana kuwa ndio njia kubwa inayosaidia kukinga Malaria.
Katika maadhimisho hayo, wananchi na vikundi
vya mazoezi wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais walifanya matembezi ya hiari
yaliyoanza Mazizini, Wilaya ya Magharibi B na kumalizia viwanja vya Maisara,
Mjini Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment