Zaidi ya Ekari 20 za msitu wa Hifadhi ya jamii wa wananchi wa
Kikunguni Shumba Viamboni, Wilaya ya
Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba zateketea na moto.
Moto huo umeiunguza zaidi ya miti 588 mikubwa, imeunguwa moto
katika msitu huo ikiwemo Mivule, Mbamba kofi , Mikorosho, Mitondoo , Mifuu , Michocha,
Mizambarau Sali, ambayo ingekatwa na kuuzwa kisheria zingepatikana zaidi ya
shilingi Milioni 20.
Msitu huo wenye ekari 50 umekubwa na majanga hayo, baada ya watu
wasiojulikana kupiga tanu ya mkaa na kuacha moto chini, uliosambaa katika msitu
huo wa jamii.
IDARA ya Misitu na Mali zisizorejesheka
Pemba, imesema imesikitishwa na kitendo kilichofanywa na watu wasio julikana,
kuchoma moto msitu wa wanajamii wa Kikunguni Shumba Viamboni
Mkuu idara hiyo harif Faki Sharif, amesema athari iliyopatikana ni
kubwa kwa kupoteza miti adimu sana, pamoja na suala
la kimazingira.
“Athari lazima zitakuwepo
na wala hazikosekani, kama unavyojuwa miti ina mambo mengi muhimu, nadhani
katika mvua hizi zinazoendelea kunyesha basi hali ya asili inaweza kurudi japo
kuwa si kwa kasi kubwa”amesema.
Amewataka wananchi kuwapiga vita watu wanaopiga tanu za mkaa, karibu
na misitu huo au karibu na majumba ili kudhibiti athari itakayoweza kujitokeza
baadae.
0 comments:
Post a Comment