November 17, 2015


Jumla ya kobe 201 waliokuwa wakisafirshwa nje ya nchi wakamatwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K Nyerere  jijini Dar es salaam.
Makobe hao walikuwa  wamehifadhiwa katika mabegi matano walikamatwa usiku wa kuamkia leo na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika huo.
Watuhumiwa waliokuwa wakisafirisha wanyamapori wametajwa kuwa ni  David Mungi mkazi wa Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman  mkazi wa Zanzibar.
Mabegi yaliyokuwa na Kobe hao yaligundulika na mbwa maalum (sniffer dogs) wa kugundua huku watuhumiwa hao walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akikagua mabegi yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii

0 comments:

Post a Comment