November 17, 2015


Tume ya  Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza idadi ya madiwani wa viti maalumu kwa vyama vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Octoba 2015.
Madiwani walioteuliwa ni 1393 kutoka katika Vyama vya CCM, CHADEMA, NCCR- MAGEUZI  pamoja na CUF huku 15 wakisubiri chaguzi ZA kata 34 zimalizike katika kata zilizosalia ili kufikisha idadi ya madiwani 1402 wa kuteuliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari  Mkurugenzi wa Uchaguzi  Ramadhani Kailima  Amesema katika madiwani hao walioteuliwa alifafanua CCM 1,021, Chadema 280, CUF 79, ACT- Wazalendo 6 na NCCR Mageuzi 6.
Amesema halmshauri ambazo bado hazijakamilisha uchaguzi zitasubiri uchaguzi ukamilike kwa kata zote ndiyo waunde baraza la halmashauri na kazi ya kwanza kwa baraza hilo ni kuchagua meya wa halmashauri husika.
Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi  NEC amesema kuwa  ni Desemba 20 mwaka huu, ndio tarehe ya mwisho wa Uchaguzi katika Majimbo na Kata zilizokuwa hazikufanya Uchaguzi .

0 comments:

Post a Comment