Bodi ya Mapato Zanzibar
(ZRB) inakusudia kuanzisha mfumo wa kulipa kodi kwa njia
ya mtandao “oline payment” ili kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara.
Afisa uhusiano wa bodi
hiyo Makame Khamis Mohamed amesema lengo ni kuhakikisha inatoa huduma bora kwa
walipa kodi ili kuwasilisha mauzo yao kwa njia za kisasa Zanzibar.
“Endapo tukifanikiwa
hatua hii ya huduma ya kulipia kwa mtandao basi ZRB tutachukua jukumu la
kuwajuilisha wafanyabiashara wetu ili kuanza kutumia mfumo huo mara moja.
Afisa mohamed amesema
mbali na kuondoa usumbufu pia njia hiyo ya mtandao italeta ufanisi katika
ukusanyaji wa kodi pamoja na kuwasilisha mrejesho kwa walipa kodi.
Hata hivyo amewaomba wafanyabiashara
wote kuendelea kutumia huduma ziliopo sasa huku ZRB ikiwa katika harakati za kuhakikisha
inaendelea kuboresha huduma hizo.
Hadi Machi mwaka 2015
ZRB Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ilikusanya mapato ya kodi ya Sh. bilioni
135.7 sawa na asilimia 95 ya makadirio
ya miezi tisa hadi kufikia mwezi huo.
0 comments:
Post a Comment