Waziri
Mkuu mteule wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa amesema hakuwa na
taarifa yeyote juu ya uteuzi wake uliofanywa na Rais.
Majaliwa
amedai usiri uliotumika ni mkubwa ambao hata yeye atauendeleza katika kuimarisha
Serikali.
“Huwezi
amini mpaka asubuhi nafanya zoezi na Wabunge wenzangu sikuwa najua lolote, mimi
ni kocha wa timu ya mpira ya Bunge”
"……Yani mpaka Spika ameanza na
ile Ruangwa nikapigwa na butwaa, na nimelia kwa sababu sikuamini kilichotokea,
ila ndo hivyo Rais ameniamini akanipa nafasi” alisema Majaliwa alipokuwa akizungumza
na Azam TV.
0 comments:
Post a Comment