Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko
kisiwani Pemba, imetakuwa kuhakikisha inapita katika masoko mbali mbali kuangalia
hali ya mfumuko wa bei za vyakula ilivyo sasa.
Mfumuko huo wa bei unadaiwa kusababishwa na wafanya
biashara, kushindwa kusafiri kwenda kufuata bidhaa nje ya kisiwa Cha Pemba kwa
kisingizio cha kutotengamaa kwa hali ya amani kutokana na uchaguzi Mkuu wa mwaka
huu pamoja na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali Tanzania.
Ali Hassan Omar mkaazi wa Chake Chake, aliyomba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia hali ya mfumko wa bei ulivyo hivi sasa,
ikilinganishwa na maisha ya wananchi walivyo.
Amina Khamis Ramadhan mfanya biashara katika soko la Matunda Chake
Chake, alisema kwa sasa wanalazimika kuuza biashara bei ya juu kutokana na kuna
wafanyabiashara wengi wamesita kusafiri kwenda kuzifuata bidhaa nje ya kisiwa
cha Pemba kama zamani.
kwa sasa kisado kimoja cha tungule kimefika shilingi 3000/= kwa
tungule za Pemba, kutoka shilingi 2000, huku zile za Tanzania bara zimefikia shilingi
4000/= kwa kisado kimoja
Hamad Haji ambaye ni msambazaji wa biashara katika soko la katari,
amesema kutokana na mvua zinazoendelea wananunua mzigo wa bidhaa za mbatatata,
vitunguu maji na tungule katika masoko ya Tanga kwa bei ya juu, hali inayowapa tabu
kuweza kuuza kwa bei ya chini wanapozifikisha kisiwani Pemba ili kupata faida.
Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla akielezea
hali hiyo amesema wafanyabiashara wamezoea kupandisha bei za vyakula, kwa
visingizio kadhaa ikiwemo upandaji wa thamani ya Dola wakati imeshashuka kwa
muda mrefuu.
0 comments:
Post a Comment