March 02, 2016

Jumla ya vyandarua 780,000 vinatarajiwa kugaiwa kwa wananchi wa wilaya zote za Zanzibar na Kitengo cha kumaliza malaria Zanzibar.
Ugawaji wa vyandarua hivyo utaanza March 16, 2016 utaanzia katika wilaya nne ikiwemo ya Magharibi A na B, Mjini na ya Mkoani  Pemb.
kazi kama hiyo ya ugawaji wa vyandarua majumbani kwa mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2012.
Akizungumza na waandishi wa habari  Mjini Zanzibar  kuhusu shughuli hiyo Mkuu wa sehemu ya uhamasishaji wa kitengo hicho Mwinyi Issa Khamis amesema wameamua kuanza katika shehia hiyo kutokana na kugundulika kuongezeka maabukizi ya malaria.
Kitengo hicho pia kimeanza upigaji dawa majumbani ambapo kiasi ya nyumba 26,336 katika shehia 45 za Zanzibar  itapigwa dawa hiyo.
Mkuu wa kazi za upigaji dawa mbu wa malariar Rashid Abdalla amesema mpango huo unalenga kufikia asilimi 85 ya idadi hiyo ili kuhakikisha wanapunguza wingi   wagonjwa Zanzibar.
Amesema kwa sasa shughuli hiyo imerahisishwa zaidi na kupelekwa kwa wananchi ambapo kumewekwa vituo maalum vya utoaji huduma kwa haraka.  
Mapema akitoa maalezo kwa waandishi wa habari  Kaimu Meneja wa kitengo cha Kumaliza Malaria Zanzibar Mwinyi Issa Mselem amesema kazi hizo  ni katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Amesema wameamua kufanya mikakati hiyo kwa kuzingatia kuwa kuzingatia kipindi cha mvua ambacho ni cha maambukizi mengi kinakaribia.

Amewaomba wananchi kuvitumia vyandarua watakavyogaiwa pamoja na kukubali kupigiwa dawa za kuulia mbu wa malaria katika vyumba yao.

0 comments:

Post a Comment