March 02, 2016

Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki umefanyika jijini Arusha nchini Tanzania ukiongozwa mwenyekiti wake Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli.
Akihutubia mkutano huo ameziomba nchi wanachama wa jumuiya hiyo kubadilika ili kufikia malengo  ya  jumuiya hiyo kwa pamoja.
Amesema kila nchi wanachama ina matatizo yake hivyo ni vyema kufanya kazi na kuvumiliana katika  kuimarisha maendeleo na ustawi wa raia na kufikia malengo ya waasisi wa jumuiya hiyo.
Dk magufuli ameitaka  sekretarieti ya jumuiya hiyo kufikiria kubana matumizi ili kusaidia matatizo mengine yanayozikabili nchi wanchama katika kuyafikia mawazo ya waanzilishi wake.
Amefahamisha kuwa nchi zote za jumiya hiyo ni masikini hivyo watendaji hao wanapaswa kubadilika kulinga na halisi ya nchi zao kwa kufanyakazi kwa manufaa ya wananchi wao.
“Ni lazima mfahamu kuwa fedha mnazozitumia ni jasho la raia masikini hivyo ni vyema tukaafikiria kuwa na matumizi sahihi kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili kwa maendeleo yao ” amesema.
Aidha ametaka kutungwa kwa sheria au kanuni kali itakayosaidia kubana upatikanaji wa michango ya wanchama wa jumuiya hiyo ambayo kwa wakati mwengine imekuwa ikichelewa  kutolewa.
katika mkutano huo wakuu wa nchi wanachama nao walizungumzia suala la kuimarisha jumuiya hiyo ambapo kwa upande wa rais Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya wamesisitiza haja ya jumuiya hiyo kufanyakazi kwa vitendo katika kuleta mabadiliko.
Nae rais wa uganda Yoweri Museveni ameelezea umuhimu wa jumuiya hiyo katika kukabiliana na ushindani na nchi nyengine duniani pamoja na kuwa na mikakati ya ulinzi na usalama wamatifa yao kwa pamoja kulingana na hali ya sasa.
Amesema inashangaza nchi wanachama wa jumuiya hiyo kila mmoja analinda usalama wa nchi yake mwenyewe wakati nchi za ulaya ambazo zimendelea kiuchumi zina umoja wao wa ulizni akitolea mfano wa jeshi la umoja wa ulaya NATO.

Mkutano huo pia umeithibitisha Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo, kumuongezea muda wa mwaka mmoja wa uwenyekiti Rais John Magufuli pamoja na kuapishwa kwa Liberat mfumukeko kuwa Kkatibu mkuu mpya wa  Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.












0 comments:

Post a Comment