March 03, 2016

Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania  TCRA  imezitoza faini ya Sh. Milioni 90 Kampuni tano za Mawasiliano ya Simu za Mkononi  kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya kanuni za ubora wa huduma.
Kampuni hizo ni Aitel imetozwa sh. milioni 22.5, Smart sh. milioni 12.5, Tigo sh.milioni 25,Vodacom sh. milioni 27.5 pamoja na Zantel sh.milioni 25.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa  TCRA Dk.Ally Simba amesema kampuni hizo zimepigwa faini tofauti kutokana na makosa mbalimbali ya utoaji huduma ya mawasiliano kwa wananchi.
Dk.Simba amesema kampuni ziliitwa na mamlaka na zilikiri kufanya hivyo na kukubali na kosa na kuafiki maamuzi ya kuwapiga faini kwa mujibu wa sharia za nchi.
Ametaja baadhi ya makosa hayo ni simu iliyopiga kudai kuwa inatumika wakati sivyo, wakati mwingine simu unapiga mwito wake unadai simu hiyo haipatikani wakati simu hiyo iko hewani.
Amesema kuwa kutokana kampuni hizo kushindwa kutimiza masharti TCRA itaendelea na utekelezaji wa sheria na maamuzi mengine kwao kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.
Dk.Simba amesema kuwa kampuni za simu za mikononi zimejikita katika kujitangaza kwa njia mbalimbali katika kuweza kupata wateja wapya lakini hazifanyi uwekezaji wa huduma bora kwa wananchi wanaotangazia.
Katika hatua nyengine TCRA imeipiga faini kampuni ya Azam Marine Sh.Milioni Tano kutokana na kufanya usafirishaji wa vifurushi kutoka Dar es Salaam na Zanzibar bila kuwa na leseni ya utoaji wa huduma hiyo.
Amesema kuwa ni kosa kwa Azam Marine kufanya huduma ya posta bila kuwa leseni huku wakikri kufanya biashara ya kusafirisha vifurushi.

Kampuni nyengine ni ya Lifalo imetozwa faini sh.milioni 10 kutokana na kufanya masafa ya ujumbe mfupi bila kuwa na kibali cha TCRA na lifalo ilikiri kufanya hivyo.
 Watendaji wa TCRA na waandishi habari wakisikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,
 Dk. Ally Simba (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment