Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB imeshindwa kufikia makadiro ya kukusanya mapato
ya zaidi ya sh. billioni 145 na badala yake imekusanya sh. bilioni 125 katika
kipindi cha July hadi January mwaka huu.
Tatizo hilo limechangiwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo wafanya biashara kutotoa risiti kwa wanunuzi wa bidhaa na
uingiaji wa bidhaa kwa magendo kupitia bandari bububu.
Meneja wa huduma kwa wateja wa bodi hiyo Ahmed Haji Saadat akizungumza katika
semina ya waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kulipa kodi amesema bodi hiyo kitendo
hicho kinaikosesha mapato serikali.
Meneja huyo amesema katika kulithibiti tatizo
hilo ZRB kwa kushirikiana na jeshi la polisi inafanya msako katika bandari hizo
pamoja na vituo vinavyouzwa mafuta ili kuwabaini wanaokwenda kinyume na
utaratibu uliowekwa.
0 comments:
Post a Comment