Jumuiya
kimataifa ya Intanational Holly of Quran Memorazation yenye makao yake nchini Saudi
Arabia inatarajia kufungua chuo cha kuhifadhia Qurani Kisiwani Pemba hivi
karibuni ilikuendeleza watoto wakislamu kujifunza kuhifadhi qurani kwa wingi visiwani humo..
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii Kisiwani Pemba Mjumbe wa tasisi hiyo Abdul Azizi al-Umiry
amesema madrsa hiyo tayari imeanza
kujengwa na inatarajia kumalizika hivi
karibuni
Amesema
ujio wao kisiwani pemba ni kutoa mafunzo kwa walimu wa madrasa na wanafunzi
walio kwisha hifadhi Quran juzuu 30 ili kutafuta mbinu bora za kuwafundisha
wanafunzi njia itakayo kuwa nyepesi kwao kuhifadhi kitabu kitukufu cha Qur an
Akizungumza
wakati wa kufungua mafunzio hayo mbunge wajimbo la Mgogoni DR Suleiman Ali Yusufu
amesema ujio wa huo ujumbe ni jitihada zinazo endelea kufanywa na jumuiya ya
kuhifadhi Quran kisiwani humo ili kufanikisha maendekleo ya kuhifahi qurani
kisiwani pemba
Ujumbe huo
unatarajiwa kuwepo Pemba kwa siku mbili na utaendelea na mafunzo kama hayo huko
Unguja
0 comments:
Post a Comment