Wavuvi
na watendaji wa ghuba ya menai wilaya ya kusini kuzifuata sheria na taratibu za
uvuvi zilizowekwa ili kuepukana na mizozo isiyo ya lazima inayojitokeza mara
kwa mara.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya uvuvi Zanzibar Mussa Aboud
Jumbe huko Makunduchi wakati akizungumza katika kikao cha kujadili mbinu za
udhibiti wa uvuvi haramu unaoendelea kwa kasi katika vijiji mbalimbali vya
kanda za pwani wilayani ya kusini.
Eneo
hilo limekuwa likikumbwa na mizozo ya mara kwa mara hasa kati ya wavuvi wa kijiji cha mtende na kizimkazi
wanaolalamikiwa kuchukuwa wageni kutoka tanzania bara na maeneo jirani kuvua
katika maeneo ya ukanda wao wa bahari.
Wavuvi hao wanadaiwa kutumia zana zisizoruhusiwa
ikiwemo mabomu na chupa za gesi hali inayowatia hofu wananchi ya kupungua kwa mazalio ya samaki na uharibifu
mkubwa wa mazingira ya bahari.
Mkurugenzi
mussa amesisitiza haja ya wavuvi na watendaji wa ghuba ya menai kuziheshimu na
kuzitekeleza vyema sheria zilizopo ili kuhakikisha vitendo hivyo vinapungua
kwenye maeneo hayo.
hata
hivyo amesema serekali kwa kushirikiana na idara yake inaendelea na jitihada za
kutafuta njia za kupambana na uvuvi haramu ili kuhakikisha rasilimali zilizopo za bahari zinatunzwa na
zinaendelea kuwanufaisha wanavijiji wenyewe.
Nae
Mkuu wa wilaya ya kusini Khamis Jabir Makame amesema serekali haitasita
kuwachukulia hatua za kisheria wavuvi au watendaji wa ghuba ya menai
watakaobainika kuenda kinyume na utaratibu.
Kikao
hicho kimewashirikisha masheha, wavuvi, wakuu wa madiko, wenyeviti na makatibu
wa kamati za uvuvi vijijini, pamoja na watendaji mbalimbali wa ghuba za Menai.
0 comments:
Post a Comment