Naibu kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali |
Amesema mbali na
kuwepo mitizamo tofauti ya kidini amani ni suala muhimu na iwapo litavunjika
kutakuwa na ugumu wa kuabudu na kuwepo kwa maendeleo.
Akifungua
mafunzo ya vijana wa dini tofauti wa Zanzibar Naibu Kadhi amesema ili kuwepo
hali hiyo ni lazima kuheshimiana na kuvumiliana mawazo, imani na haki ya kila
mtu na kusaidia kuepusha mizozo isiyo na
lazima.
Nae mchungaji Stanley
Nicholas Lichinga amewataka vijana kuwa mabalozi wazuri katika kujenga
maridhiano pamoja na kuwa makini katika matumizi ya teknolojia kwa misingi ya
kuheshimu dini na utamaduni.
Akitoa maelezo
mratibu wa jukwaa la maridhiano ya dini Daniel Nygaard amesema viongozi wa dini
wana nafasi kubwa ya kuwa na umoja katika kuzungumzia suala la amani katika
mahubiri yao katika jamii.
0 comments:
Post a Comment