Serikali imesema
haipo tayari kuona karafuu ya Zanzibar inapoteza
hadhi na ubora wake kutokana na kuchafuliwa na baadhi ya watu wasiokuwa
waaminifu.
Kauli hiyo imetolewa
baada ya kutolewa malalamiko juu ya kupunguzwa uzito na kuchanganywa na vitu
visivyohitajika kwa karafuu zinazosafirishwa nje ya nchi.
Naibu katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo na Mali asili Zanzibar Juma Ali Juma akizungumza katika semina
ya ubora wa zao hilo huko Pemba amesema
hatua zitachukuliwa kudhibiti
hali hiyo na wanapaswa kusimamia ni wakaguzi na wapasishaji katika vituo vya
manunuzi.
Amesema wizara
hiyo itaweka utaratibu wa kuwabaini watendaji watakaofanya uzembe ama kula
njama katika kutekeleza wajibu wao wa kazi.
Nae Mkurugenzi Mwendeshaji
wa shirika la Biashara la Taifa Zanzibar ZSTC Mwanahija Almas Ali amesema wamefanikiwa
kupata mashine ya kupima ubora wa karafuu kwa majaribio na iwapo itafanikiwa
zitawekwa katika vituo vyote vya manunuzi.
0 comments:
Post a Comment