November 18, 2015


Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wa barabara ya Bumbwini Kikobweni mkoa wa kasakzini Unguja.
Barabara hiyo hiyo ina urefu wa klm 4.3 ipo katika hatua za mwisho za uwekaji wa kifusi na zaidi ya klm 3 zimeshaekewa kifusi utagharimu zaidi ya milioni mia tatu kwa hatua hiyo.
Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dkt Juma Malik Akil amesema Serikali inakusudia kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami lkn kwa sasa itajengwa kwa hatua za kifusi tu.
"Licha ya kuwepo mvua nyingi katika maeneo hayo lkn kazi za ujenzi huu wa barabara  unaaendelea kama kawaida ili kila mtu aweze kufaidi huduma hiyo muhimu" amesema Dkt Juma.
Sambamba na hayo aliwataka wananchi wa kijiji hicho kutumia vyema miundombinu hiyo idumu kwa muda mrefu zaidi. 
Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dkt Juma 
Malik Akil akipewa maelezo na Eng Cosmas kuhusu ujenzi wa 
barabara ya Bumbwini Kikobweni unaoendelea kwa hatua ya kifusi

0 comments:

Post a Comment