November 18, 2015


Shirika la biashara la Taifa  Zanzibar ZSTC lina mpango wa kutoa usajili wa kudumu kwa wakulima wa zao la karafuu wa Zanzibar.
Mpango huo ni juhudi za kupata idadi halisi ya mashamba yanayolimwa zao hilo katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
Mkurugenzi wa mfuko wa maendeleo ya karafuu Zanzibar Ali Suleiman Mussa amesema shirika hilo pia limo katika matayarisho ya kuanzisha bima kwa wakulima ili watakapo pata ajali wapatiwe mafao kwa haraka.
Amefahamisha kuwa mikakati hiyo inaweza kulisaidia shirika kujua mahitaji ya wakulima na kuwatambua wananchi wanaomba mikopo mikubwa ya kuendeleza mashamba ya mikarafuu kwa udanganyifu.
Alikuwa akizungumza na watendaji wa wilaya  nne za pemba ikiwemo  wete, micheweni, chake chake  na mkoani ikiwa  ni mwendelezo wa mikutano mbalimbali  ya uhamasishaji na uendelezaji wa zao la karafuu visiwani Zanzibar.
Zao la karafuu ni zao kuu la biashara linalotegemewa sana katika uchumi wa visiwa hivi ambapo kwa sasa Serikali ya Zanzibar imekuwa ikichukuwa juhudi ya kulimaarisha zao hilo ili kuongeza uzalishaji.

0 comments:

Post a Comment