November 18, 2015

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itagharamia zoezi la marudio ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kutokana na hitilafu.
Katibu Mkuu Wizara ya fedha wa  SMZ Khamis Mussa Omar amesema uchaguzi ni suala la kikatiba na ndio dira ya  uendeshaji wa nchi hivyo wizara hiyo itahakikisha inagharimia fedha zinazohitajika kwa a ajili ya kuendesha zoezi hilo.
“Masikio yetu na wananchi wote tunaelekeza kwa tume ya uchaguzi itamke lini uchaguzi huo utafanyika ili wizara  itekeleze wajibu wake” alisema.
Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amesema serikali haingilii na inaheshimu mamlaka ya tume ya uchaguzi iliyopewa na katiba ya Zanzibar ya 1984  na iwapo ikihitaji mahitaji yote yaliyopo kisheria itatoa.
Tume  ya  Uchaguzi  Zanzibar  uliofanyika octoba 25 kwa madai ya kuwepo dosari  nyingi  ikiwemo uchaguzi  kutokuwa  huru  na  wa haki. 
Hata hivyo chama kikuu cha upinzani Zanzibar CUF kimekuwa kikirejea kauli yake mara kwa mara kuwa haitashiriki katika uchaguzi wa marejeo ambao hadi sasa tarehe yake haijatangazwa na badala yake wanataka ZEC ibadilishe maamuzi yake na kuendelea kutangaza matokeo hayo.

zanzibarleo


0 comments:

Post a Comment