November 03, 2014


Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi amesema  anachukizwa na tabia ya viongozi wa upinzani ya kujaribu kuupotosha umma kwa kumwita msaliti wa kuuza ardhi ya Zanzibar, Tanzania bara.
 Amesema kitendo hicho cha udhalilishaji kinaonyesha dharau kubwa anayofanyiwa na inastahiki kuchukuliwa hatua.  
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wanachama wa ccm jimbo la Koani huko Unguja Uuuu wilaya ya kati amesema suala hili linazungumzwa kimakosa na hakuna kipengele kinachoelezea ardhi ya Zanzibar kuhodhiwa na Muungano katika  katiba iliyopendekezwa.
Akitoa ufafanuzi aliekuwa Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba ambae pia ni Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati  Ramadhan Abdalla Shaaban   amesema kilicho kuwemo ndani ya katiba hiyo ni kutoa fursa kwa kila mtanzania kumiliki ardhi katika sehemu ya Jamuhuri ya Muungano endapo katiba hiyo itapita.

Amesema katika mfumo huo Serikali ya Zanzibar itakuwa na haki ya kupanga au kusimamia matumizi ya ardhi ya visiwani Zanzibar wakati ile ya bara itasimamiwa na Serikali ya Muungano mfumo  utakaompa haki Mtanzania yeyote kutumia ardhi hiyo.

Mapema katika mkutano huo balozi Seif alidai kuwa CCM  itashinda uchaguzi wa mwaka 2015 na kitauzika upinzani unaoonekana kushindwa kuongoza dola tokea kuanzi kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania  katika miaka ya 90.

0 comments:

Post a Comment