Taasisi zinazosimamia masuala ya udhalilishaji zimelalamikiwa kwa utendaji mbaya unaohusishwa na rushwa na hivyo kuchangia kuendelea kwa vitendo hivyo.
Wakichangia katika mkutano wa kutathmini utekelezaji wa mradi wa (GEWE) baadhi ya waandishi wa habari wa vyombombalimbai vya Zanzibar wamesema hatua hiyo ni pamoja na ucheleweshwaji wa kesi na kutolewa hukumu ndogo kwa watuhumiwa.
Wamesema mbali na jamii kuwa na mwamko wa kuriroti matukio hayo iwapo tabia hizo kwa watendaji wa polisi na mahakama hazitapigwa vita juhudi za kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji zitashindikana.
Wamesema kwa sasa tatizo kubwa linaikabili jamii kuhusiana na vitendo vya ulawiti kwa wanafunzi wa skuli mbalimbali masual ambayo hajaibuliwa kw akiwango kikubwa
waandhishi hao wameshauri kutafutwa mbinu za kuishinikiza serikali kuweka mkazo katika kuharakisha upatikanaji wa mashine ya dna na mabadiliko ya sheria zinazokwamisha utoaji haki ikiwemo ya ushahidi ambayo imepitwa na wakati.
Akitoa maelezo afisa wa mradi wa GEWE Asha Abdi amewashauri waandishi kuibua taarifa zaidi za matukio ya udhalilishaji pamoa na kuonesha kasoro za kiutendaji hasa kwa taasisi za mahakama na polisi kwa lengo la kuharakisha mabadiliko.
Mradi huo wa GEWE ulilenga kujenga uwezo wawanwake katika kusimamia na kutetea haki zao dhidi ya vitendo vya udhalilishaji wa kinjinsia ulikuwa unatekelezwa katika Mikoa mitatu ya Zanzibar kwa mashirikiano na serikali ya Denmark.
0 comments:
Post a Comment