October 10, 2014


Zanzibar leo imeungana na nchi nyengine duniani kuadhimisha siku ya wagonjwa akili duniani ambapo ongezeko la wagonjwa hao ni kubwa lilofikia zaidi ya elfu 4800 katika kipindi cha mwaka 2013 hadi juni 2014.
Wagonjwa hao wameripotiwa katika vituo vya afya mbali mbali ikiwemo Kidongo chekundu, Kivunge, Pwani mchangani na hospitali ya Makunduchi pekee iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja imepokea wagonjwa 2498
Mratibu  wa afya ya akili zanzibar Dk Suleiman Abdu Ali amewaambia waandishi wa habari kuwa ingawa sababu ya matatizo hayo haijafahamika lakini wengi wao wanachangiwa na  matumizi ya dawa za kulevya, urithi, na msongo wa mwazo na wasiwasi.
Amefahamisha kuwa mbali na ongezeko hilo la wagonjwa utoaji wa huduma za bado ni changamoto kutokana na uchakavu wa majengo, dawa na vifaa vya kufanyia kazi inayotokana na uhaba wa  bajeti .                                                                        
Muuguzi wa wagonjwa  katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya kidongo chekundu  Bai Kumvi Juma amewaomba wazazi kuwa tayari kutoa misaada kwa wagonjwa hao ili kuwalinda na matatizo ya kijamii
Siku ya afya ya akili duniani huadhimishwa kila ifikapo October 10, na kauli mbiu ya mwaka huu ni JAMII IISHI NA WAGONJWA WENYE MATATIZO MAKUBWA YA AKILI.

0 comments:

Post a Comment