Kamisheni ya Utalii Zanzibar imeandaa mikakati mipya
ya utalii na kuacha kutegemea zaidi nchi za Ulaya kwa kuandelea kujitangaza
zaidi kiutalii katika masoko mapya ya
nje ya nchi ili serikali kukuza uchumi wake.
Amesema
Kupanuka kwa soko hilo kutasaidia kuondokana na utegemezi wa soko la nchi za bara
hilo ambazo zinakabiliwa na changamoto kadhaa hali iliyopunguza mchango wa kwa
sekta ya utalii.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na
kuanzishwa kwa safari ya ndege ya Ukraine hapa Zanzibar, Naibu katibu mkuu wa
wizara hiyo Issa Mlingoti amezitaja baadhi ya nchi ziliomo katika masoko hayo
mpya yanayochipukia na wamepanga kuyafikia kikamilifu ni china, india, Israel,
urusi na Ukraine
Amebainisha
kuwa takwimu za uingiaji watalii kutoka nchi hizo ndani ya kpindi cha miaka
iwili 2014 -2015 imwapa moyo na nguvu inayohitajika ni kasi ya kujitangaza
zaidi
‘Israeli
wageni wake wanatembelea Zanzibar wamefikia 7546 kutoka 3818 na , wageni kutoka
Poland wameongezeka kutoka 3163 hadi 4083 katika kipindi hicho chs miaka miwili’,
amsema Mlingoti.
Amefahamisha
kuwa katika mpango huo wa kujitangaza zaidi Febuari 12 ndege ya kwanza
inatarajiwa kuingia Zanzibar moja kwa moja kutoka Ukraine itashusha watalii 250
ambao watakaa Zanzibar kwa kiindi cha siku tisa.
Naibu
Mlingoti ameeleza kuwa ndege hiyo imedhaminiwa na na kuletwa na kampuni ya
Traveling Profession Group kutoka Ukraine kwa kushirikiana na Sun Tours and Travel Zanzibar.
Amesema
wanategemea ndege hiyo itafanya safari zake hizo za Zanzibar mwaka mzima kama
kutakuwa na mafaniko zaidi.
0 comments:
Post a Comment