February 11, 2016


STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE

 Zanzibar                                                                                                                                    11.2.2016
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha  Ndugu Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu (Uwezeshaji), katika Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto.
Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee.
Wengine ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib  pamoja na Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo ndugu Hassan Khatib Hassan alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,
Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Asha Abdalla  baada ya
kumalizika kwa hafla ya kuapishwa Hassan Khatibu Hassan kuwa
 Naibu  katibu wizara hiyo leo katika Ukumbi wa Ikulu
Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi waliohudhuria katika
 hafla ya kuapishwa kwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi
 wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Hassan Khatib  Hassan leo 
 katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, kabla alikuwa
Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba,[Picha na Ikulu.]


Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

0 comments:

Post a Comment