Shirika la nyumba Zanzibar limeandaa mpango wa
kuwatoza ada ya usafi wananchi wanaoishi nyumba za maendeleo za Michenzani hasa katika kukarabati
makaro yao ili kuepusha maradhi ya mripuko.
kwa sasa shughuli za usafi katika nyumba hizo zinategemea fedha kutoka Serikalini kitendo kinachokwamisha shughuli za usafi katika majengo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Mohammed Hafidh
Rajab amesema utaratibu huo utasaidia kuzuia kero ya kuziba kwa
makaro katika maeneo hayo.
Amesema shirika la nyumba limeamuwa kufuata
utaratibu unaotumika katika mji mkongwe ambao umefanikisha mji huo unakuwa
katika hali ya usafi na kuwa ni kivutio kizuri kwa watalii wanaofika nchini.
Akizungumza kuhusu ubovu wa
makaro katika nyumba namba 5 michenzani amesema tatizo hilo linatarajiwa
kurekebishwa hivi karibuni kutokana na upatikanaji wa zaidi ya shilingi milioni
20 kutoka mfuko wa serikali zitakazotumika kufanya marekebisho katika
nyumba za Michenzani..
0 comments:
Post a Comment