Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi
|
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imewateua makada watatu watakaowania kuchaguliwa kugombea nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la 11 kupitia chama hicho.
Walioteuliwa
kugombea nafasi hiyo na Kamati Kuu iliyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM,
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni pamoja na Naibu Spika aliyemaliza
muda wake JOB NDUGAI, Dkt. TULIA ACKSON na ABDULAH MWINYI.
Wana-CCM
hao watatu watapigiwa kura na Kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM
kitakachofanyika kesho Novemba 16, 2015 saa nne asubuhi katika ofisi za Makao
Makuu ya CCM Dodoma ilikuchagua jina moja kugombea nafasi hiyo katika Bunge la
Jamhuri ya Muungano.
Kwa
upande wa Naibu Spika wa Bunge, mchakato wa kuchukua fomu kwa wabunge wa CCM
wanaoomba ridhaa kugombea nafasi hiyo utaanza kesho Novemba 16, 2015 na
kukamilika Novemba 17, 2015 saa kumi kamili jioni.
Hadi jana nafasi ya
Naibu Spika mwanachama mmoja tu ndiye aliyekuwa amechukua fomu ya kugombea nafasi
hiyo ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu,’ lakini kutokana na kasoro
za kanuni atatakiwa kuchukua fomu upya.
CCM blog
0 comments:
Post a Comment