November 15, 2015


Ongezeko kubwa la wagonjwa wa kisuakari Zanzibar linatishia kupungua kwa nguvu kazi ya taifa. 
Daktari bingwa wa kisukari kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja amesema Faidha Kassim Suleiman amesema takwimu zinaonyesha kuwa kwa sasa kiasi ya wagonjwa 7000 wameripotiwa kuwa na ugonjwa huo visiwani hapa.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani amesema waathirika wa kisukari Zanzibar wanaongezeka kwa kasi kutokana na jamii kutokuwa na mpangilio bora wa chakula kwa kula vyakula visivyo na faida au tiba mwilini.
Dokta Faidha amearifu kuwa tiba pekee ya kujikinga na kisukari ni pamoja na kuwa na mfumo bora wa maisha , kufanya mazoezi, kula kwa wakati na kutumia vyakula vyenye afya.
Aidha amegusia tatizo la watu wanaougua kisukari  kushindwa kufuata miiko na masharti ya ugonjwa huo hali inayowasabishia wengi wao kufariki dunia mapema au wengine kukatwa viungo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ‘ ni mlo gani unaotakiwa kwa mgonjwa wa kisukari”

0 comments:

Post a Comment