TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salam za
pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Mbwana
Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza
Barani Afrika; iliyotolewa katika mji wa Abuja nchini Nigeria jana usiku.
Mhe.
Rais Magufuli amemtaka Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa
mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Amesema
tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe,
wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.
Aidha,
Rais Magufuli amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo kuongeza
juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za kimaendeleo.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
08
Januari, 2016
0 comments:
Post a Comment