Masheha wa shehia za Kojani Mkoa wa wa Kaskazini
Pemba wametakiwa kuzuia ufanywaji wa biashara za majimaji ili kuzuia kuenea kwa
ugonjwa wa kipindupindu. Amri hiyo ameitolewa na Mkuu wa Mkoa huo Omar Khamis
Othman alipotembelea kambi ya kipindupindu na kuelezea kusikitishwa na baadhi
ya wananchi kuendelea kuuza biashara hizo zilizopigwa
marufuku.
Jumla ya wagonjwa 24 wa kipindupindu wamelazwa
katika kambi hiyo tangu kuzuka kwa ugonjwa huo.
Amesema ni vyema kwa masheha na kamati zao
za afya kuhakikisha biashara za maji maji haziuzwi hasa katika kipindi hiki cha mripuko
wa ugonjwa wa kipindupindu.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka masheha
kuondoa muhali katika kufanikisha agizo hilo kwa kuwachukulia hatua
za kisheria wanaokaidi kutekeleza agizo hilo.
Kwa uapde wake Afisa wa afya kitengo cha
magonjwa ya mripuko Said Khatib Juma amesema kuwa Wizara ya Afya kwa
kushirikiana na masheha imeunda timu itakayofanya msako wa nyumba zinauza juisi na malai ili kuzichukulia hatua.
0 comments:
Post a Comment