November 15, 2015


 Rais wa Tanzania Dr John Magufuli amemtumia salamu za pole Rais wa Ufaransa François Hollande, kutokana na mashambulizi ya kigaidi yaliyosababisha vifo vya watu 127.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rais Magufuli amesema Serikali ya Tanzania inaungana na wapenda amani duniani kulaani tukio hilo lililopoteza maisha ya watu wengi.
Kikundi cha wanamgambo wa ISIS kimesema kimehusika na mashambulizi hayo.
Mlipuko wa kujitoa muhanga uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa Stade de France eneo watu walikuwa wakiendelea kusherehekea tamasha la muziki huku timu za taifa za Ujerumani na Ufaransa zikicheza mechi ya kimataifa, na kusababisha Rais Francois Hollande kuondolewa uwanjani.
Mamlaka zimewataka wananchi kutotoka nje, huku Jiji la Paris likiwa limefunga majengo mengi ya umma na kuongeza ulinzi wa kijeshi.

0 comments:

Post a Comment