Serikali imebaini wizi
wa takribani shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World
Travel iliyopo visiwa vya Komoro.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.
“Kufuatia upotevu huo Serikali imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha usalama mtandaoni ili kubaini mtandao mzima uliohusika” amesema Prof. Mbarawa.

Aidha ameongeza kuwa kwa
utaratibu wa kawaida wa shirika hilo wakala anapewa ruhusa
ya kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na
pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa
tena.
Prof. Mbarawa anasema
kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua
kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.
“Siku mbili zilizopita
nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na
hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi
kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya
utumishi wa umma” amesema Prof. Mbarawa.
Vilevile ameongeza kuwa
Serikali imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha
za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.
Prof. Mbarawa ametoa
wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa njia ya mtandao kwa kuwa
sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha kuwa
watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa hatua stahiki. :Maelezo
0 comments:
Post a Comment