Bodi ya Elimu Mkoa wa Kusini Pemba
imesema tatizo la wanafunzi wa Mkoa huo kufanya vibaya katika mitihani ya Taifa
iliyopita ya mwaka 2015 linachangiwa na uzembe wa baadhi ya walimu, wanafunzi na wazee katika kusimimia
maendelo ya masomo.
Imeongeza pia uwezo mdogo wa walimu kufundisha, uhaba wa walimu
wa fani mbali mbali hasa masomo ya Sayansi huku pia baadhi ya walimu wanaonekana
hawana hamu ya kazi hiyo.
Bodi hiyo katika kikao chake chini ya
Mwenyekiti wake Omar Khamis Ameir kilijadili matokeo ya mtihani wa kidato cha
nne na kutoa wito kwa pande zote zinazohusika na maendeleo ya elimu katika
Skuli mbali mbali zijitahidi kutekeleza wajibu wao ili matokeo yajao yawe
mazuri.
Aidha wamependekeza kuangaliwa mfumo
wa utoaji wa ajira za walimu ili kupata walimu bora wanaofanya kazi kwa umakini
zaidi.
Wakati huo huo Bodi hiyo imeikagua
Skuli ya Sekondari ya binafsi ya Farahedy iliopo Mkoroshoni iliyoomba usajili
wa kudumu na kupendekeza kupatiwa usajili huo kutokana na kukidhi vigezo.
Msimamizi wa Skuli hiyo Sheikh Saleh
Omar amesema tatizo la kukosa usajili wa kudumu limekuwa ni kikwazo kwa Skuli
hiyo kupata wanafunzi wa kutosha na msaada kutoka sehemu mbali mbali.
0 comments:
Post a Comment