Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein amesema kila mtu
anajukumu la kuelimisha Jamii kuhusu utamiaji wa matumizi ya mitandao ya
Kijamii kueleza faida na hasara zake.
Amesema ipo baadhi ya
mitandao hiyo inatumiwa kurusha habari za uchochezi na uongo dhidi ya serikali
huku wakijua taarifa wanazozituma zinapingana na sheria na maadili ya nchi.
Akizungumza katika
maadhimisho ya siku ya sheria katika viwanja vya Victoria Garden Dkt amefahamisha
kuwa ingawa kila mtu sheria zimeonesha kua kila mtu ana haki ya kupata habari
na kutoa habari bila ya kubughudhiwa lakini taarifa hiyo isivunje sheria zilizo
wekwa.
“Mitandao ni nyenzo muhimu katika maisha ya Binaadamu iwapo
itatumika vizuri haitakuwa na hasara hivyo kuna haja kwa kila mmoja kuelimisha
jamii yake umuhimu wake na hasara zake”amesema Dkt Sheni.
Ameeleza kuwa Tanzania imetunga
sheria ya mitandao ya mwaka 2015 yenye lengo la kuimarisha matumizi bora kwa
kuainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya teknolojia ya habari.
Amesema sheria hiyo
itaanza kutumika Zanzibar baada ya kuridhiwa na Baraza la Wawakilishi hivyo
ametoa wito kwa taasisi zinazohusika na utoaji taaluma ya sheria kuongeza kasi
ya kuwa elimisha wananchi juu ya sheria hiyo mpya.
Amewahimiza majaji, mahakimu,
wanasheria na jeshi la polisi kuisoma sheria hiyo na kuielewa ili waweze kutoa
mchango wao katika kuitekeleza kwa
mujibu wa majukumu na nafasi zao.
Kuhusu uimarishaji wa
huduma za mahakama Dkt Shein ameahidi kuwa ujenzi wa mahakama kuu mpya
unaotarajiwa kufanyika huko Tunguuu Mkoa wa kusini Unguja utaaanza katika mwaka
ujao wa fedha.
Amefahamisha kuwa bajeti
ijayo ujenzi wa mahakama hiyo utaanza bila pingamizi yoyote sambana na ujenzi
wa mahakama ya watoto tayari wametengewa milioni 30 za kukamilisha jengo hilo.
0 comments:
Post a Comment