STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 22.1.2016
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo ameongoza mazishi ya marehemu Bi Asha
Bakari Makame aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Mazishi ya
Marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman yalifanyika huko Kianga, Wilaya ya Magharibi
‘B’, Mkoa wa Mjini Magharibi kwa heshima zote za Chama Cha Mapinduzi, ambapo
viongozi mbali mbali wa vyama na serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif
Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd.
Wengine
waliohudhuria ni Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dk.
Mohammed Gharib Bilal pamoja na Rais wa Zanzibar mstaafu Dk. Amani Abeid Karume
na wananchi.
Mapema asubuhi, Alhaj
Dk. Shein alifika nyumbani kwao marehemu huko Jangombe, mjini Unguja kwa ajili
ya kutoa mkono wa pole kwa wana familia pamoja na kumuombea dua marehemu.
Baada ya hapo
Alhaj Dk. Shein alishiriki katika dua maalum (hitma) pamoja na sala ya kumsalia Marehemu Bi Asha Bakari Makame iliyofanyika
huko Masjid Noor Mohammad, Mombasa kwa Mchina mjini Unguja.
Akisoma wasifu
wa Marehemu, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa
Marehemu Bi Asha Bakari Makame alizaliwa Disemba 12 mwaka 1949 huko Mtambwe,
Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Kwa mujibu wa
maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Marehemu Bi Asha alipata elimu ya
msingi huko huko kijijini kwao Mtambwe na baadae alijiunga na Skuli ya
Sekondari ya Fidelcastro huko Kisiwani Pemba hadi Kidato cha nne ambapo baada
ya hapo alienda nchini Bulgaria kwa ajili ya kujiendeleza kwa elimu ya Diploma
ya Siasa na Utawala.
Vuai alieleza
kuwa tokea uhai wake, Marehemu Bi Asha Bakari Makame, akiwa skuli na baada ya
kumaliza skuli alikuwa akijishughulisha na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Afro
Shirazi Party (ASP) na baadae alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pale kilipoanzishwa
mnamo mwaka 1977.
Katika uhai wake
Marehemu Bi Asha Bakari Makame, aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi
pamoja na Serikali ikiwemo Naibu Waziri, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo
ambapo pia, aliwahi kuwa Waziri wa Wanawake na Watoto.
Marehemu Bi Asha
Bakari, alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa
mnamo mwaka 1983 na baadae alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo
nafasi aliyoendelea nayo hadi kufa kwake.
Naibu Vuai
katika akisoma wasfu huo wa Marehemu alisema kuwa marehemu Bi Asha katika maisha yake alikuwa muumini wa kweli
wa Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 pamoja na kuwa muumini wa kweli wa
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika mwaka 1964.
Marehemu Bi Asha
Bakari Makame, katika kipindi chake chote alichotumikia chama cha CCM pamoja na
serikali alikuwa kiongozi muaminifu, muadilifu, mchapakazi na asiyeyumba katika
masuala ya msingi.
Naibu Vuai
alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatoa mkono wa pole kwa ndugu na jamaa
wote wa marehemu. Nao wanafamilia walitoa shukurani Kwa wale wote waliohudhuria
mazishi hayo.
Marehemu ameacha
watoto watatu, wakiwemo wawili wa kike na mmoja wa kiume Mwenyezi Mungu aiweke
roho ya marehemu mahala pema peponi. Amin.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449.
Fax: 024 2231822 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
0 comments:
Post a Comment