January 22, 2016

Tume ya uchaguzi wa Zanzibar ZEC imetangaza tarehe ya uchaguzi mkuu wa marejeo ambapo utafanyika machi 20.
Taarifa ya tume hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa wake Jecha Salim jecha kupitia zbcc radio imeleza kuwa Uchaguzi huo utahusisha nafasi ya urasi wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani na hakutakuwa na mikutano ya kampeni za wagombea.
“Katika kikao chake cha terehe 21 Jan 2016 uchaguzi utafanyika Jumapili tarehe 20 March 2016”
Ameongeza kuwa wagombea wote walioteuliwa awali wataendelea kuwa wagombea wa nafasi hizo.
Matokeo  ya uchaguzi wa Zanzibar yalifutwa oktoba 28, 2015 baada ya kugundulika kasoro nyingi.
Jecha amewashukuru wananchi kwa kuwa wastahmilivu katika kipindi chote cha kusubiri matokeo hayo.


0 comments:

Post a Comment