December 01, 2015

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza kufuta posho za Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za vikao vya kamati zao za kisekta ili kupunguza matumizi yasiyokuwa na lazima.
Huo ni miongoni mwa mipango yake ya  kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili fedha zitumike kuimarisha huduma za jamii.
Akitangaza uamuzi huo jana Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru amesema kuwalipa posho ya vikao vya bodi ni kufanya malipo mara mbili kwa kazi moja wakati vikao hivyo ni sehemu yao ya kazi.
Pia vikao vya bodi za mashirika ya umma vimepunguzwa hadi kufikia vikao vinne tu kwa mwaka. 
Msajili Mafuru alitoa agizo hilo katika mkutano na wakuu wa taasisi na mashirika ya umma na pia wenyeviti wa bodi zao na kueleza kuwa limetolewa na Rais Magufuli na kinachotakiwa ni utekelezaji wake.

0 comments:

Post a Comment