Wakati
dunia ikiadhimisha siku ya ukimwi Duniani
Tume ya UKIMWI Zanzibar ZAC imeandaa mkakati wa tatu wa kitaifa wa
kumaliza maambukizi ya UKIMWI ifikapo 2030.
Mkakati
huo utakwenda sambamba na utekelezaji wa programu maalum kwa watu wanaoishi na
virusi vya ukimwi ili kujitambua kwa
asilimi 90 ifikapo 2020.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ZAC Dk Ali Salim Ali ametoa
taarifa hiyo maalum ya Serikali katika kuadhimisha siku ya UKIMWI
inayoadhimishwa kila ifikapo Disemba 1 na kwa mwaka huu ikiwa na kauli mbiu “Tumia
fursa zilizopo katika kumaliza UKIMWI duniani”.
Akizungumzia
kuhusu hali ya maradhi hayo Zanzibar amesema tafiti zinaonesha kuwa wanawake
wanaojiuza miili yao na watumiaji wa
dawa za kulevya ndio wanaongoza kwa mambukizi kwa asilimia 10 kuliko
kundi makundi mengine ya kijamii
zanzibar.
Dkt
Ali ameongeza kuwa utafiti huo uliofanyika
kupitia mpango wa muda mfupi wa ZAC wa
mwaka 2007 na 2012 pia umebaini karibu watu 4000 wanajiuza na wengine
kiasi ya watu 3000 wanajidunga sindano na wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na
wengine ni vijana wa umri kati ya miaka 15 hadi 16 Zanzibar.
Amesema
kupitia mpango huo kumekuwa na mafanikio katika upimaji wa hiari wa mama na
mtoto mbapo kwa sasa Zanzibar ina vituo
156 ikilinganishwa na vituo 137 vya mwaka 2012 vinavyotoa huduma za ushauri
nasaha na upimaji na upimaji wa hiari kwa mama wajawazito.
Hata
hivyo Mkurugenzi Ali amesema bado UKIMWI ni tishio duniani ikiwemo Zanzibar hivyo
juhudi zinapaswa kuchukuliwa ili kufikia matarajio ya kuijenga Zanzibar bila ya
UKIMWI.
0 comments:
Post a Comment