December 01, 2015

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi kuamini kuwa Serikali ipo na inaendelea na kazi za kuwahudumia wananchi.
Amesema hayo alipotembelea mradi wa maji huko Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema utekelezaji wa mradi huo ni miongoni mwa kazi inazofanya ili kuwapatia huduma ya uhakika ya maji safi katika kipindi kifupi kijacho.
Dk. Shein amesema visima vitatu vimechimbwa vitapeleka maji katika tangi hilo kubwa lililobadilishwa kupitia mradi wa Ras el Khaimah ili kusambaza maji ya kutosha kwa matumizi ya wananchi.
Waziri  wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban amebainisha kuwa kazi ya ulazaji wa mabomba kutoka kisima kipya cha pango la Mnywambiji huko Kibuteni iko mbioni na imebakia sehemu ndogo kukamilika.
Mradi huo wa ubadilishaji wa tangi pamoja na uchimbaji wa kisima kipya huko makunduchi unatekelezwa kwa ushirikiano wa SMZ, Uongozi wa Jimbo, Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation pamoja na wananchi.

0 comments:

Post a Comment