December 01, 2015


Kiasi ya shilingi bilioni 5 zimetengwa kwa ajili ya utanuzi wa barabra ya Mwanakwerekwe makubaburini hadi  Fuoni kituo cha polisi yenye urefu wa kilomita 4.
Barabara hiyo itajengwa na Idara ya ujenzi na utunzaji wa barabara Zanzibar UUB na fedha hizo ni makusanyo ya kodi za wananchi kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.
Mhandisi Mkuu wa utunzaji wa barabara Zanzibar Cosmas Masolwa amesema kwa sasa idara imenza kazi ya kutanua upana wa barabara na baadhi ya nyumba zitavunjwa.
Hata hivyo ameeleza kwa wananchi wanaovunja au kuvunjiwa nyumba hizo hawataliwa fidia yeyote kwa kuwa walikiuka masharti ya ujenzi na kuvamia hifadhi ya barabara.
Mhandisi Msolwa amesema idara taarifa zilikuwa zinatolewa kwa wananchi waliokuwa wanajenga ndani ya hifadhi ya barabara lakini wengi yao walikaidi amri hiyo.
Amefahamisha kuwa barabara hiyo ilikuwa inaharibika mara kwa mara hivyo imelazimika kufanyiwa matengenezo kutokana na uchakavu uliozidi.
Mbali na mradi huo pia inaendelea na miradi mengine ya barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami ukiwemo ule wa barabara ya Bungi muembe kiwete wa kilimoita  2.2, Chuo cha utalii ndani wenye urefu wa mita 400 na wa Chuo cha Fedha Chwaka wa kilomita moja na mengine iko Pemba.

0 comments:

Post a Comment