Mradi mkubwa wa
Kimataifa wa ujenzi wa kisiwa cha Kitalii kitatengezezwa kwa mfumo wa
ufukiaji Bahari umeanza rasmi katika eneo la Hoteli ya Utalii iliyopo Mtoni
Marine kaskazini Magharibi ya Mji wa Zanzibar.
Hata
hivyo gharama kamili za Mradi huo bado hazijafahamika hadi utakapokamilika
rasmi ujenzi wake hapo baadaye.
Mradi
huo unaoendeshwa na Kampuni ya Kizalendo ya Bakhresa Group utahusisha
ujenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Ghorofa Tano ya Daraja la Tano (Five
Star+), eneo la wazi la mapumziko pamoja na kutengeneza Kisiwa cha Mji
mpya .
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi kampuni hiyo Said Salim Bakhresa amesema ujenzi wa mradi huo ni muhimu
kwa uchumi na utasaidia mapato ya Taifa
pamoja na kutoa ajira kubwa kwa vijana wazalendo.
Nae
Mhandisi wa Mradi huo Ahmed Shamsi amesema ujazaji wa mchanga katika eneo
linalofukiwa unafanyika kwa kutumia chombo maalum chenye uwezo wa
kunyonya na kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari na kukata
Majabali.
Amefahamisha kuwa kazi ya uchimbaji na kufukia
mchanga katika eneo hilo zilianza Mwezi uliopita wa Novemba zinatarajiwa
kukamilika mwezi ujao wa January.
Akitoa nasaha zake
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipitembelea kuangalia kazi hiyo amemupongeza Uongozi wa Bakhresa
Group kwa uamuzi wa kuanzisha mradi huo mkubwa uliozoeleka katika Mataifa
yaliyoendelea ambao utakapo kamilika utasaidia kuitangaza Zanzibar na Tanzania kiutalii
Kimataifa.
Mfumo
huo wa ufukiaji Bahari kwa ajili ya kuanzisha miradi ya Kiuchumi ni mfumo
unaotumiwa na Mataifa mbali mbali Duniani na kwa Afrika mradi kama huo
umeshafanyika katika Kisiwa cha Seycheles.
Sehemu inayoendelea kufukiwa hapo Mtoni Marine ambayo itatumika hapo baadaye kwa ajili ya eneo maalum litakalotoa fursa kwa Wananchi kupata mapumziko . |
Othman Khamis Ame
Ofisi
ya Makamui wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/12/2015.
0 comments:
Post a Comment