April 23, 2014

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inaipitia sheria za elimu kutokanana kukwamisha usimamiaji wa maendeleo ya mtoto wa kike.
Mrajisi wa wa elimu Zanzibar Siajabu Suleiman Pandu amesema sheria hizo ikiwemo ya elimu ya mwaka 1982 inahitaji marekebisho makubwa kwani zimeweka ugumu wa kufuatilia wanaokwamisha haki ya watoto kupata haki ya elimu.
Ameeleza kuwa moja ya kasoro zilizokuwemo ni adhabu dhaifu kwa wazazi wanaowafungusha ndoa watoto wao wakati wakiwa masomoni.
Sheria hiyo imeweka faini ya shilingi 1500 kwa mzazi anayefanya kosa hilo adhabu aliyodai inayosababisha kuendelea kwa tabia hiyo na hata ugumu wa kufuatilia kesi hizo.

Mrajisi huyo amesema wameamua kufanya marekebisho hayo tena baada ya yale ya awali ya mwaka 2010 kupitwa na muda na hata hayajachukuliwa hatua licha ya kuwepo sera ya elimu sera ya elimu ya mwaka 2006.
Akizungumzii juu ya marekebisho ya sheria ya wari na wajane ya mwaka 2005 amesema wizara hiyo inakusudia kuangalia mfanikio yaliyofikiwa tangu ilipoanza kutekelezwa.
Mrajis Sijabu ametoa takwimu za wanafunzi waliopata ujauzito na kuolewa tangu kuanza kutumika sheria hiyo hadi 2013 ambapo waliolewa 591 na walipewa ujauzito ni 364.
Ameyaeleza hayo katika mafunzo ya udhalilishaji wa kijinsia kwa waandishi wa habari yanayoendeshwa na TAMWA kwa udhamini wa mfuko wa ruzuku kwa vyombo vya habari Tanzania TMF.


1 comment: