Jumla ya kesi 31 za makosa ya jinai
yaliyofanywa na watoto zimewasilishwa katika mahakama mbalimbali za mkoa wa Mjini
Magharib kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Kati ya kesi hizo kesi 2 zimepatiwa
dhamana, kesi 1 imekutwa na hatia na kesi 7 zimefutwa kutokana na kukosekana
ushahidi.
Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa
marekebisho ya tabia kwa watoto wanaovunja na walio katika hatari ya kuvunja sheria Zanzibar
inaonesha tatizo la makosa ya jinai kwa watoto ni kubwa katika Mkoa wa mjini Magharibi ikilinganisha na mikoa mengine.
Mradi huo wa mwaka mmoja na nusu
umefadhiliwa na shirika la kimataifa la UNICEF na kutekelezwa na taasisi Kituo cha huduma za sheria Zanzibar Z.L.S.C
na tanzania youth icon TAYI chini ya usimamizi wa idara ya ustawi wa jamii Zanzibar.
Akitoa taarifa hiyo mratibu wa mradi Abdallah
Ahmed Sleiman kutoka kituo cha huduma za sheria Zanzibar amesema wanawasaidia watoto
huduma za kisheria pamoja na kuwawakilisha watoto mahakamani.
Afisa kitengo cha ustawi wa jamii Nyezuma
Said Issa amewataka watekelezaji wa mradi huo kuongeza juhudi za utoaji wa
elimu, kutumia vyema rasilimali ili kupunguza tatizo hilo.
Nayo kamati ya hifadhi ya mtoto ya Wilaya
ya mjini imeomba kuendelezwa ushirikiano wa wadau katika ngazi zote ndani ya wilaya na
kuwa karibu na familia kwa kuwa ni njia pekee ya kubaini vyanzo na sababu zinazowafanya
watoto kufanya makosa.
0 comments:
Post a Comment