December 09, 2015


Jumla  ya watoto 96,000 kati ya watoto 135,000 waliofikia umri wa masomo ya maandalizi hawakuandikishwa kuanza masomo hayo Zanzibar.
Watoto hao ni sawa na asilimia 71 ya makadirio ya uandikishaji watoto waliofikia umri wa miaka minne yaliyowekwa katika bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar ya mwaka 2015.
Mratibu wa Elimu ya makuzi ya watoto wadogo ECD Pemba Haji Ali Hamad amesema kati ya watoto hao walioandikishwa watoto 18,000 waliandikishwa katika skuli za serikali na 20,000 waliojiunga katika skuli za binafsi.
Ameeleza hayo katika mkutano wa wadau mbali mbali uliokuwa mbinu za kumjenga mtoto kiakili katika umri mdogo, ulioandaliwa na Madrasa Early Child Program in Zanzibar.
Ameeleza kuwa uandikishaji wa watoto skuli umekuwa mdogo kutokana na uelewa mdogo wa wazazi wenye watoto waliofikia umri wa miaka minne juu ya umuhimu wa elimu ya maandalizi.
Mratibu Hamad amefahamisha kuwa hali hiyo imekuwa kikwazo kwa watoto hao wakati wanapotaka kuedelea na elimu ya msingi na hata elimu ya juu.
Hivyo amesisitiza taaluma zaidi inahitajika kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano ili kupata kizazi bora kilichotayarishwa vyema kielimu.
Aidha, amewataka wazazi wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuwapeleka skuli, ili kupata taaluma inayohusika na uelewa wao.

0 comments:

Post a Comment