UMOJA wa Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi UVCCM umesema unaunga mkono kasi ya utekelezaji kazi wa serikali
ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli na kinachofanyika sasa ndio
chachu ya maendeleo ya Watanzania.
Umesema utaendelea
kumuunga mkono katika kila hatua kwa lengo la kuona vijana wote wa Tanzania
wanarudi katika ari ya uwajibikaji kama ilivyokuwa wakati wa serikali ya awamu
ya kwanza.
Aidha, umesema
kinachofanywa sasa ni ni kutekeleza kwa vitendo sera za CCM
zilizoainoshwa katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020 .
Kaimu Katibu Mkuu wa
UVCCM, Shaka Hamdu Shaka amesema hayo mara baada ya kumaliza kazi ya
usafishaji mazingira katika maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru wa
Tanganyika mara baada ya kuongoza usafi huo katika eneo la la
Kigogo,jijini Dar es Salaam.
Amesema Dk. Magufuli
katika mikutano yake yote ya kampeni wakati akiomba kura kwa wananchi, aliahidi
kuongozwa na sera za Chama, malengo na mikakati itakayoleta maendeleo ya kweli.
Amesema kuwa
Mafanikio hayo na kasi ya Dkt. Magufuli ya
utendaji kamwe haiwezi kutenganishwa na ubora wa sera zilizomo katika ilani ya
uchaguzi ya CCM.
Kwa mujibu wa
Shaka, UVCCM itaendelea kumuunga mkono kwa vitendo Dk. Magufuli katika malengo
ya serikali yake hasa kupiga vita rushwa, maonevu, ubadhirifu wa mali za umma,
mkakati wa udhibiti na matumizi bora ya rasilimali na maliasil za Taifa na
kuhimiza uwajibikaji maeneo ya uzalishaji mali.
Kuhusu kasi
ya serikali katika
kuwachukulia hatua watendaji wazembe, kuwaweka kando wale wenye
tuhuma za ufujaji na wizi wa fedha za serikali, shaka amefafanua wakati wa kuoneana muhali au
kubebana umekwisha na sasa ni kazi kwenda mbele.
Katika kuunga mkono agizo
la Rais Magufuli kaimu katibu mkuu huyo amemesahuri makatibu wote wa
mikoa na wilaya kulifanya zoezi hilo kuwa endelevu na kila juma mosi ya mwisho
wa mwezi kuwa siku ya usafi utakakuwa ukisimamiwa na Vijana wote
nchini.
0 comments:
Post a Comment