Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati imetia
saini kazi ya ujenzi wa mradi wa maji na usafi wa mazingira katika mji wa Zanzibar
utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 34 zilizotolewa mkopo na benki ya Maendeleo
Afrika ADB.
Utaiji wa saini wa utekelezaji wa mradi huo umefanyika
kati ya mamlaka ya maji Zanzibar ZAWA na kampuni ya ujenzi kutoka Iran
kwa kushirkiana na kampuni ya Spencon Service limited ya Tanzania ambapo serikali
ya Zanzibar itachangia asilimia kumi tu
ya fedha hizo.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo mradi huo unatarajia
kaunza hivi karibuni utahusisha ujenzi wa matangi ya maji katika maeneo ya Saateni
na Mnara wa mbao, uchimbaji wa visima 10 vipya, kukarabati visima 20 vya zamani
na kulaza kilomita 68 mabomba ya kusambazia maji
Akizungumza katika hafla ya utaiji saini Mkurugenzi
mkuu wa ZAWA Dk Mustapha Ali Garu amesema lengo kuu ni kuhakikisha usambazaji
wa huduma ya maji inafikia wananchi kwa asilimia 90 katika mji wa Zanzibar.
Waziri wa ardhi na makaazi Ramadhan Abdalla Shaaban
amesema serikali kwa sasa inakusudia
kutafuta vyanzo mbadala vya usambazaji wa maji safi na salama ili kukabiliana
na upungufu wa huduma hiyo Zanzibar.
Hivyo mradi huo wa usambazaji wa maji katika
mji wa Zanzibar ni kuhakikisha inafikia lengo hilo kikamilifu na kuondosha
usumbufu wa kuoatikana huduma hiyo kikamilifu.
0 comments:
Post a Comment