THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
SALAMU
ZA PONGEZI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kufuatia
kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika salamu hizo Malkia wa Uingereza amemueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli
kuwa “Natumaini kuwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo
ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea wakati wa utawala wako, nakutakia
kheri pamoja na wananchi wa Tanzania” amesema malkia katika
salamu zake.
Salamu pia zimetoka kwa Mfalme Akihito wa Japan ambaye amemueleza Mhe.
Rais Dkt. Magufuli “Nakutumia salamu za dhati, mafanikio na
furaha kwako Mheshimiwa Rais na watu wa nchi yako” Amesema.
Salamu zingine kwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya
kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi, Mhe. Mohamed Abdelaziz ambaye
amemtakia kheri Mhe. Rais Dkt. Magufuli na kumueleza kuwa “Nina
imani kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea vyema chini ya
uongozi wako kuelekea katika kupata
maendeleo na mafanikio zaidi”. Amesema; na pia amekipongeza
Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa uchaguzi wa kidemokrasia ulioendeshwa
katika mazingira ya kistaarabu chini ya usimamizi wa waangalizi kutoka kwenye
kanda, bara na kimataifa na hivyo kuliletea sifa bara la Afrika.
Mhe.
Rais Dkt. Magufuli pia amepokea salamu kutoka kwa Rais wa Namibia Mhe. Hage
Geingob na kumueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa salamu zake na zile za
wananchi wa Namibia ni za dhati kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa
ushindi wa kiti cha Urais.
“Pia
napenda kutoa pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi kwa ushindi uliopatikana katika
uchaguzi wa Oktoba 25, 2015”. Amesema na kuongeza kuwa “Kwa
hakika Watanzania wamezungumza na kukipa tena CCM Mamlaka ya kuipeleka
mbele Tanzania kuelekea kwenye mafanikio zaidi”. Ameongeza.
Salamu zingine ni kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amesema
Tanzania kwa mara nyingine tena imedhihirisha kuwa ni nguzo ya demokrasia
barani Afrika.
Naye
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck amemtakia Mhe.
Rais Dkt. Magufuli na Watanzania kwa ujumla mafanikio katika kuendeleza
Taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment