Kukosekana matumizi bora ya ardhi kumeiathiri jamii kukosa uhalisia wa maeneo pamoja na
mmong’onyonko wa ardhi kisiwani Pemba .
Mkurugenzi mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya Uhifadhi Misitu
ya Jamii Pemba Mbarouk Mussa Omar
amesema hali hiyo imechangiwa na mtumizi mabaya rasilimali hasa zile
zinazoizunguka jamii.
Amewashauri wananchi kisiwani humoa kufuata maelekezo ya matumizi bora ya ardhi ili kuzuia athari zinazoendelea
zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Amefahamisha kuwa matumizi bora ya rasilimali hiyo ni pamoja na na
kupanda miti katika maeneo ya wazi na kubadilika kuanza kutumia nisahti mbadala
.
Afisa kilimo mseto wa asasi hiyo iliyopo huko Gando Ali Hamad amesema kwa sasa wanahamasisha jamii
kuanza kujihusisha na kilimo mseto kma njia ya kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi .
0 comments:
Post a Comment