November 16, 2015


Wabunge wateule wa Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho (Novemba 17,2015) wanatarajia kuanza kikao mkoani Dodoma huku wanachama nane wa vyama tofauti vya siasa wakipitishwa kuwania kiti cha uspika wa bunge hilo.
Kamati ya Wabunge wateule wa CCM imempitisha Job Ndugai kugombea nafasi ya uspika wa bunge hilo baada ya wagombea wawili waliokuwa wanachuana nae kujitoa.
 Nanyo Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umemteua, Goodluck Ole Medeye (Chadema) kusimama katika nafasi ya uspika,huku katika nafasi ya unaibu Spika akiteuliwa, Magdalena Sakaya wa Chama Cha Wananchi (CUF).
Wagombe wengine wa nafasi hiyo ya usipika wa bunge la kumi na moja la Tanzania yaliyopokelewa na Katibu wa Bunge Dr.Thomas Kashilila ni  pamoja na Peter Sarungi (AFP). Hassan Kisabiya, (N.R.A),Dkt Godfrey Malisa (CCK), Richard Lymo (T.L.P), Hashimu Rungwe (CHAUMA) na Robert Kisinini (DP).
Goodluck Ole Medeye CHADEMA
Job Ndugai CCM

0 comments:

Post a Comment