WANAFUNZI 151 wengi wao chini ya umri wa miaka 18 wamelazimika
kukatishiwa masomo yao baada ya kufungishwa ndoa hapa Zanzibar katika kipindi
cha miaka minne.
Taarifa ya Wizara ya
elimu iliyotolewa na Mrajisi wa elimu
Zanzibar Siajabu Makame Pandu, zinaeleza kuwa idadi hiyo ni wale walioripotiwa,
mara baada ya kuolewa kuanzia mwaka
2011 hadi mwezi septemba mwaka huu .
Kwa mujibu wa taarifa
hiyo mwaka 2011 kuliripotiwa wanafunzi 53, wakati mwaka 2012 wanafunzi 50 huku mwaka
2013 walifikia watoto 29 huku mwaka 2014 wanafunzi 18 wameripotiwa kuolewa.
Wilaya ya Micheweni
ilikuwa ikiongoza kuwa na idadi ya wanafunzi 62, ikifutiwa wilaya za Wete Pemba
na Kati kwa unguja wanafunzi 19, chini ya wilaya Magharibi iliokuwa na watoto
17, huku wilaya za Chake chake na Mkoani zikiwa na wanafunzi 14 kila wilaya.
Mrajisi wa elimu
Zanzibar Siajabu Makame Pandu, amesema ndoa za utotoni zimekuwa zikiathiri sana
maendeleo ya watoto wa kike kielimu, jambo linalowavunjia mipango na mikakati
yao ya baadae katika maisha.
Mrajisi wa elimu Zanzibar Siajabu Makame Pandu |
“Lazima jamii iendelee
kushirikiana na wizara ya elimu, katika kumaliza tatizo, na moja ni kiziripoti
kesi hizo wanapogundua wazazi wamewaoza waume watoto wao’’,alisema
Afisa elimu na mafunzo
ya amali wilaya ya Micheweni Mbwana Shaame, amesema huwenda kama malezi ya
pamoja yakirudi na mtoto kulelewa na jamii, hali hiyo itapungua.
Mkuu wa Mkoa wa
kaskazini Pemba Omar Khamis Othuman, amesema lazima jamii ifikirie mara mbili,
umuhimu wa kumsomesha mtoto wa kike, bada ya kuunga mkono kwenye kumuozesha.
Mratibu wa FAWE
Zanzibar, amesema moja ya sababu ya wazazi kuwaoza watoto wao, umaskini na hasa
wa kumuendeleza mtoto bado ni changamoto.
Nae Mratibu wa mradi wa
Kukuza Usawa wa kijinsia na Kuwawezesha Wanawake ‘GEWE’ kutoka Chama cha
waandishi wa habari Tanzania TAMWA ofisi ya Zanzibar, Asha Abdi Makame, amesema
mashine ya DNA pia ikiwepo inaweza kupunguza ubakaji kwa watoto. Haji Nassor, Pemba
0 comments:
Post a Comment