Ofisi
ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar imesema matumizi ya teknolojia ya
kisiasa katika kuimarisha mfumo wa takwimu ni njia pekee itakayosaidia kuandaa
sera na kupanga mipango bora ya maendeleo ya taifa.
Kufanya
hivyo kutasaidia kuwa na mfumo wa pamoja wa upatikanaji wa taarifa zenye
uhakika na kutoa viashiria mbalimbali vya kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya Zanzibar.
Kaimu
Mkurugenzi wa idara ya huduma za Kitakwimu na kiufundi wa ofisi hiyo Ali Idrisa
Shamte amewaambia waandishi wa habari katika hafla ya maadhimisho ya siku ya
takwimu Afrika yenye kauli mbiu “Takwimu bora kwa maisha bora”.
Amesema
kauli mbiu hiyo inatilia mkazo kwa wazalishaji wa takwimu kuzalisha takwimu
bora na kwa wakati kulingana na vigezo na miongozo kutoka kwa afisi hiyo ya Serikali
ya Zanzibar.
Kaimu
Mkurugenzi Shamte Amesema hatau hiyo
itasaidia katika kuwa na taarifa sahihi za katika kuandaa sera na mipango yao
mbalimbali kwa maendeleo ya taifa.
Amefahamisha
kuwa ofisi hiyo inaendelea kutoa viashiria mbalimbali kutipia tafiti kwa ajili
ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Zanzibar ikiwemo Dira ya Maendeleo ya
2020, mkakati wa MKUZA na malengo ya
Milenia ya mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment