May 16, 2014

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi ameunda tume ya watu sita kuchunguza uvujaji wa mapato katika baraza la mji la Wete.
Uamuzi wa kuunda  tume hiyo itayoongozwa na afisa manunuzi katika mkoa huo  Ali Munir Khalfan umelenga  kudhibiti ukusanyaji wa mapato wa baraza hilo ambapo kume kuwako na  taarifa kwamba mapato ya baraza hilo yemekuwa yakiishia mifukoni  kwa wachache .
Akizungumza baada ya kuunda tume hiyo Mkuu wa mkoa Dadi ameitaka kufanya kazi kwa uadilifu na kuacha kuacha muhali kwa watendaji watakaobainika kuhusika na hujma hizo.
Amesema wajumbe wa tume hiyo watakuwa na jukumu la kupita kwenye maduka ya wafanyabiashara na kuangalia uhalali wa leseni zao pamoja na viwango vya leseni wanavyokata kwa baraza hilo .
Naye mkuu wa wilaya ya Wete Omar Khamis Othman amewataka wafanyabiashara kushirikiana na wajumbe wa tume hiyo wakati itakapopita kwenye maduka yao.

0 comments:

Post a Comment